Zaidi ya watu 40 wadaiwa kuuwawa na Boko Haram, Nigeria

Wakazi wa Nigeria waondoka makwao kutokana na ghasia, kwenye picha ya maktaba.

Familia kadhaa Kaskazini Magharibi na Kati mwa Nigeria ukiwemo mji mkuu Abuja p wanaendelea kuomboleza kutokana na mauaji ya jamaa zao yaliyofanywa na washukiwa kutoka kundi la kigaidi la Boko Haram.

Watu wasio pungua 40 wameuawa kwenye mashambulizi makali dhidi ya jamii mbali mbali katika wilaya ya Zango Kataf, katika majimbo ya Kaduna na Katsina, Kaskazini Magharibi mwa Nigeria.

Wimbi jipya la ghasia limeongeza kiwango cha wasiwasi miongoni mwa wakazi wakati wanapojiandaa kupiga kura badaaye wiki hii, kwenye uchaguzi wa magavana na wabunge wa majimbo.

Mashambulizi dhidi ya eneo la makazi ya Chinkakune na kutoka kwa wateka nyara wenye silaha kali, yamesababisha vifo vya watu 5 na kutekwa nyara kwa wengine 10 ambao walipelekwa msituni, wakiwemo watoto wa chini ya umri wa miaka 6. Baadhi ya wakazi wanadai kuwa polisi walichukua muda mrefu zaidi kuwasaidia baada ya shambulizi kutokea.

Collins Atohengbe VOA, Lagos Nigeria.