Zaidi ya watu 200 waandamana Afrika Kusini kupinga mswaada wa LQBTQ uliopitishwa Uganda

Maandamanao wa watu wa jamii ya LQBTQ nchini Uganda kwenye picha ma maktaba.

Zaidi ya watu 200 Afrika Kusini wameandamana Jumanne nje ya Ubalozi wa Uganda, kupinga mswaada uliopitishwa na wabunge  dhidi ya wapenzi wa jinsia moja hivi karibuni.

Kwa mijibu wa shirika la habari la AP maandamano hayo yaliongozwa na chama cha upinzani za Afrika Kusini cha mrengo wa kushoto cha Economic Freedom Fighters, kikimuomba rais wa Uganda Yoweri Museveni kutotia saini mswaada huo kuwa sheria.

Wanaharakati wa LQBTQ pia walijiunga kwenye maandamano hayo wakishinikiza serikali ya Afrika Kusini itoe tamko dhidi ya mswaada huo, unaohatarisha uhuru na usalama wa jamii ya LQBTQ nchini Uganda.

Ushoga ni marufuku nchini Uganda, lakini mswaada huo unapendekeza kuongeza adhabu kali kama vile hukumu ya kifo pamoja na kifungo cha miaka 20 jela. Karibu wabunge wote 389 wa Uganda waliuunga mkono mswaada huo ambao sasa unasubiri iwapo Museveni atautia saini na kuwa sheria.