Ukatili huo ulianywa na vikosi vya usalama vya taifa hilo la Afrika Magharibi, dhidi ya wapinzani wa dikteta wa muda mrefu Yahya Jammeh. Makundi ya wanaharakati yamepongeza kesi hiyo dhidi ya Ousman Sonko ambaye alikuwa waziri wa mambo ya ndani, kati ya 2006 na 2016, chini ya utawala wa Jammeh, kama fursa ya kufikia hukumu kwenye mahakama ya kimataifa, inayoruhusu kuendeshwa mashitaka ya ukatili uliotekelezwa kwenye taifa la kigeni.
Sonko mapema Jumatatu alifikishwa kwenye mahakama ya jinai katika kusini wa Bellinzona. Kiongozi huyo alikuwa ameomba hifadhi nchini Uswizi Novemba 2016, lakini alikamatwa miezi miwili baada ya kuingia nchini humo. Ofisi ya wendesha mashitaka nchini Uswizi imesema mashitaka dhidi ya Sonko yaliwasilishwa mwezi Aprili na yanajumuisha ukatili uliotekelezwa wakati wa utawala wa Jammeh wa miaka 16, ambao uligubikwa na ukamataji holela, unyanyasaji wa kingono, pamoja na mauaji ya kiholela.