Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken anabadili mwelekeo wake kwenye mazungumzo ya usalama na Mexico baada ya kufanya kazi kutuliza uhusiano na mshirika wake Ufaransa.
Baada ya kusimama Alhamisi katika jimbo la California Blinken anaungana na Waziri wa Usalama wa Ndani wa Marekani Alejandro Mayorkas na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Merrick Garland huko Mexico City kwa kile wizara ya mambo ya nje inakiita mazungumzo ya ngazi ya juu ya maswala ya usalama.
Atakayewakilisha upande wa Mexico atakuwa waziri wa Mambo ya nje Marcelo Ebrard na mawaziri wa ulinzi na usalama.
Ebrard alisema mapema wiki hii anataka kuiona Marekani ikiwasafirisha watuhumiwa kwenda Mexico haraka zaidi, ili kuzuia mtiririko wa bunduki kutoka Marekani kuingia Mexico na kuboresha juhudi za kufuatilia mtiririko wa fedha zinazotumiwa na taasisi za kihalifu.