Waziri wa Mambo ya Nje Rubio atangaza balozi wa Afrika Kusini hatakiwi nchini

  • VOA News

Ambassador Ebrahim Rassol (Source: Social Media Twitter).

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio ametangaza kuwa balozi wa Afrika Kusini kwa Washington hatakiwi nchini wakati uhusiano wa nchi hizo mbili ukidorora.

Rubio ameandika katika mtandao wa X akisema kuwa balozi wa Afrika Kusini kwa Marekani Ebrahim Rasoo “kamwe hakaribishwe katika nchi yetu kubwa.”

“Ebrahim Rasool ni mwanasiasa mbaguzi wa rangi ambaye anaichukia Marekani na kumchukia @POTUS (Rais wa Marekani).”

Hakuna majibu ya haraka kutoka ubalozi wa Afrika Kusini mjini Washington D.C.

Hatua imekuja huku kukiwa na uhusiano kati ya Marekani na Afrika Kusini. Rais Donald Trump hivi karibuni alitia amri ya kiutendaji kusitisha misaada kwa Afrika Kusini juu ya sheria yenye utata ya mageuzi ya ardhi ambayo Trump anasema itapelekea kuchukua mashamba yanayomilikiwa na wazungu. Trump pia alisema kuwa wakulima wa Afrika Kusini wamekaribishwa kuishi nchini Marekani.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa aliandika mtandao wa X alitetea hatua za serikali.

“Tunaongozwa na Katiba, ambayo inaweka jukumu kwa serikali kuchukua hatua za kurekebisha athari za ubaguzi wa rangi hapo awali,” alisema.

“Tumeelezea wasi wasi kuhusu tabia mbaya ya hali nchini Afrika Kusini na sheria zetu fulani na misimamo ya sera zetu za mambo ya nje,” Ramaphosa alisema baada ya Trump kutia saini amri ya kiutendaji.