Amesema kwamba hilo ni kulinganishwa na makundi mengine ya waandamanaji, na kwa hivyo kuongeza mgogoro wa kisiasa uliyosababishwa na vita kati ya Israel na Hamas.
Kwenye shambulizi lisilo la kawaida dhidi ya polisi, waziri Suella Braveman amesema kwamba idara ya polisi ya London ilikuwa ikizembea katika kuwajibisha uvunjaji wa sheria kutoka kwa waandamanji wanaounga mkono Palestina.
Braveman aliwataja waandamanaji hao wanaoitisha sitisho la mapigano huko Gaza kuwa wenye chuki. Waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak yupo kwenye shinikizo la kumfukuza kazi Braveman anayeonekana kuleta migawanyiko kwenye kitengo chenye nguvu ndani ya chama tawala cha Kikonsavative.