Kuleba ameyasema hayo mbele ya wanahabari mjini Islamabad akiwa na mwenzake wa Pakistan Bilawal Bhutto Zardari ,katika siku ya kwanza ya ziara yake rasmi ya siku mbili, ikiwa ya kwanza kufanywa na waziri wa mambo ya nje wa Ukraine tangu kurejeshwa kwa ushirikiano wa kidiplomasia kati ya mataifa yote mawili 1993.
Mkataba wa nafaka wa Black Sea uliongozwa mwaka jana na UN na Uturuki, na kuondoa vizuizi kwa nafaka kwenye bandari za Ukraine ambavyo viliwekwa na Russia, baada ya kuivamia nchi hiyo, Februari mwaka jana.
Jumatatu Moscow ilitangaza kujiondoa kwenye mkataba huo ambao umesifiwa kwa kudhibiti upungufu wa chakula pamoja na mfumuko wa bei kwenye mataifa mengi yanayotegemea nafaka kutoka Ukraine.