Waziri wa fedha Uganda amekamatwa kwa madai ya kuiba mabati

Mary Goretti Kitutu, mmoja kati ya mawaziri wanaoshtakiwa kwa ufisadi wa mabati eneo la Karamoja huko Uganda. April 6, 2023.

Mabati yalitengwa kwa ajili ya makazi ya gharama nafuu huko Karamoja eneo ambalo halina maendeleo na halifuatiliwi huko kaskazini magharibi mwa Uganda linapakana na Kenya na Sudan Kusini.

Waziri wa fedha wa Uganda Amos Lugoloobi amekamatwa kwa madai ya kuiba mabati yaliyowekwa kwa ajili ya eneo maskini na tete polisi imesema Jumamosi.

Mabati yalitengwa kwa ajili ya makazi ya gharama nafuu huko Karamoja eneo ambalo halina maendeleo na halifuatiliwi huko kaskazini magharibi mwa Uganda linapakana na Kenya na Sudan Kusini.

Mary Goretti Kitutu waziri anayehusika na eneo la Karamoja pamoja na maendeleo yake akiwa na kaka yake walishtakiwa kuhusiana na kesi hiyo hapo Aprili 4. Kulingana na polisi zaidi ya mawaziri 10 wa serikali, wabunge 31 na maafisa 13 wa serikali wanachunguzwa katika kesi hiyo.

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine anasema mashtaka dhidi ya Kitutu ni mwanzo wa ufisadi kamili na aliishutumu serikali ya rais Yoweri Museveni ambaye amekuwa madarakani kwa muda mrefu kwamba inaelekea kubaya.