Video nyingine inamuonesha waziri huyo, ambaye anawania kiti cha ubunge cha jimbo lililo kaskazini mwa Uganda akishiriki katika mchakato wa kisiasa bila kufuata kanuni za wataalamu wa afya zinazosisitiza watu kutokaribiana sana.
Dkt Aceng hata hivyo amejitetea akisema kuwa alikuwa akiufundisha umma namna ya kuvaa barakoa.
Licha ya kauli yake, wakososaji wanasema alitakiwa kufuata kanuni za serikali, ikizingatiwa kwamba baadhi ya Waganda wamefariki na wengine wamewekwa gerezani kwa kukiuka taratibu hizo.
Wazoiri Aceng anafahamika nchini kote kwa kuongoza kampeni ya mapambano dhidi ya COVID-19 na hata amepewa jina la utani la “Mama Corona.”
Matangazo ya umma anayotoa akiwasihi watu kuvaa barakoa na kufuata kanuni za kutokaribiana kati ya mtu mmoja hadi mwingine yamekuwa yakirushwa hewani na vyombo vya habari nchini.
Peter Magelah, mwanasheria wa haki za binadamu wa shirika lisilo la kiserikali la “Chapter Four” anasema waziri huyo anatakiwa kufahamu muongozo “wetu unaoeleza kwamba baadhi ya waganda wanafikiri virusi hivi ni ulaghai, na vinatumiwa kwa ajili ya mafanikio ya kisiasa.”
“Watu wamekamatwa, watu wamefyatuliwa risasi na kuuawa kwa kutokufuata muongozo uliotolewa na kutiwa saini na Waziri Aceng. Halafu kuna mtu ambaye ni kioo cha kuhamasisha watu wafuate kanuni hizo, ambaye ndiye anakiuka kanuni ambazo zimepelekea baadhi ya watu kufa,” alisema Magela katika mahojiano na VOA.
Ripoti katika eneo zinasema watu wapatao 10 wameuawa na vikosi vya usalama kwa kukiuka miongozo iliyowekwa ili kudhibiti kusambaa kwa COVID-19. Uganda hivi sasa ina zaidi ysa kesi 1,000 zilizothibitishwa za ugonjwa huo.
Waziri wa Habari, Judith Nabakooba, anasema Waganda wanatakiwa kuvaa barakoa wanapokuwa hadharani kulingana na muongozo wa wizara ya afya.
“Tunajutia tukio hilo. Kwa sababu tunafahamu vyema miongozo inatangazwa mara kwa mara na tunategemea kwamba kila mmoja atafuata kanuni hizi. Hata hivyo, hilo lisiwe suala la kuomba samahani kwa Waganda kumtumia waziri huyo kama mfano wa kutelekeza miongozo iliyopo,” alisema.
Katika taarifa yake, waziri Aceng anaeleza kwamba alikuwa hafanyi mkutano wa kisiasa kama ilivyodaiwa, lakini alikuwa anasambaza vyandarua na barakoa.
Anasema wafuasi wake walimkimbilia kumsalimia na ilikuwa vigumu kuwadhibiti ambapo wengi wao walitaka kupata barakoa za bure au kupiga picha naye.
Waziri huyo anasema anafahamu vyema taratibu na kanuni za serikali zilizowekwa za kusitisha kusambaa COVID-19 na anawasihi Waganda kufuata muongozo huo.