Waziri mkuu wa Ethiopia athibitisha kuondoka kwa wanajeshi wake, Mekelle

Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed

Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amekiri kwamba wanajeshi wa serikali yake wameondoka katika mji mkuu wa jimbo la Tigray, Mekelle baada ya miezi kadhaa ya mapigano..

Kiongozi huyo amesema hatua hiyo ni kutokana na kuwa wameondoka na kuwa mji huo haukuwa tena kiini mizozo.

Afisa mwingine wa serikali amesema wanajeshi wanaweza kurudi huko katika wiki zijazo ikiwa itahitajika. Ni taarifa ya kwanza ya maafisa wa serikali kuu tangu vikosi vya chama cha People’s Liberation Front (TPLF) kuchukua udhibiti wa mji huo mapema wiki hii.

Hata hivyo msemaji wa TPLF ameyataja maelezo ya waziri mkuu kuwa yasiyo ya kweli, akisema wanajeshi wa serikali kuu walishindwa vita na ndipo waliondoka Mekelle.

Ameongeza kuwa wanajeshi wa Eritrea ambao ni washirika wa serikali kuu hawajaondoka huko Tigray kama alivyodai afisa mmoja wa Ethiopia hapo awali.