Watu wawili wamejeruhiwa katika shambulio la risasi Jerusalem

Polisi wa Israeli katika mojawapo ya maeneo yaliyokuwa na ghasia huko Jerusalem, Jan. 25, 2023.

Shambulio la Jumamosi linakuja chini ya saa 24 baada ya watu saba kuuawa kwa kupigwa risasi na mpalestina aliyekuwa bunduki  katika sinagogi kwenye viunga vya  Jerusalem. Watu 10 walijeruhiwa katika shambulio la Ijumaa kabla ya polisi kuwasili na kumuua mtu huyo mwenye silaha

Watu wawili walijeruhiwa katika shambulio la risasi Jumamosi mjini Jerusalem.

Shambulio la Jumamosi linakuja chini ya saa 24 baada ya watu saba kuuawa kwa kupigwa risasi na mpalestina aliyekuwa bunduki katika sinagogi kwenye viunga vya Jerusalem. Watu 10 walijeruhiwa katika shambulio la Ijumaa kabla ya polisi kuwasili na kumuua mtu huyo mwenye silaha.

Shirika la habari la Associated Press linaripoti kuwa mshambuliaji wa Jumamosi alipigwa risasi na polisi, lakini hali yake haikubainika mara moja.

Siku ya Alhamisi, uvamizi wa jeshi la Israel katika kambi ya wakimbizi huko Jenin, uliua watu tisa, moja ya siku za umwagaji damu zaidi huko Ukingo wa Magharibi kwa miaka mingi.

Maafisa wana wasiwasi kuwa mashambulizi hayo huenda yakawa mwanzo wa kuongezeka kwa mashambulizi nchini Israel na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.