Watu tisa wamekufa kufuatia mlipuko katika jengo huko Russia

Mfano wa mlipuko katika jengo lililolipuka hivi karibuni huko Russia

Mlipuko huo katika kisiwa cha Sakhalin cha Pasifiki cha Russia ulionekana kusababishwa na mitungi ya gesi iliyofungwa kwenye jiko la kupikia kulingana na mashirika ya habari ya Russia

Mlipuko katika jengo la ghorofa tano mashariki mwa Russia umesababisha vifo vya takriban watu tisa, wanne kati yao wakiwa watoto, maafisa walisema Jumamosi.

Mlipuko huo katika kisiwa cha Sakhalin cha Pasifiki cha Russia ulionekana kusababishwa na mitungi ya gesi iliyofungwa kwenye jiko la kupikia kulingana na mashirika ya habari ya Russia.

Wafanyakazi wa dharura wanaendelea kuwatafuta manusura chini ya vifusi, maafisa walisema.