Watu 7 wameuawa na wengine 22 wametekwa nyara nchini Nigeria

Jimbo la Borno lililopo nchini Nigeria

Ukosefu wa usalama ni wasi wasi mkubwa katika taifa hilo lenye watu wengi barani Afrika wakati Rais mpya anatarajiwa kuapishwa mwezi huu kufuatia uchaguzi ulioibua utata kutoka kwa upinzani.

Watu saba wameuawa na 22 wengine wametekwa nyara katika mashambulizi mawili tofauti katika jimbo la kaskazini mashariki la Borno nchini Nigeria mahala ambako makundi ya wanajihadi yanaendesha harakati zao vyanzo vya usalama na wakaazi wamesema Jumamosi.

Ukosefu wa usalama ni wasi wasi mkubwa katika taifa hilo lenye watu wengi barani Afrika wakati Rais mpya anatarajiwa kuapishwa mwezi huu kufuatia uchaguzi ulioibua utata kutoka kwa upinzani.

Siku ya Alhamis wakulima watatu waliuawa na 11 wengine walitekwa nyara na wanaoshukiwa wanajihadi wa Islamic State West Africa Province (ISWAP) karibu na kijiji cha Bulayobe kuelekea mji wa Banki vyanzo vilisema.

Wakulima waliingia kilomita 10 nje ya Banki kusafisha mashamba kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa kupanda mazao wakati mvua za kila mwaka zinatarajiwa baada ya siku kadhaa.