Takriban watu 60 waliuawawa na wengine kadhaa kujeruhiwa siku ya Jumatatu katika mlipuko uliotokea katika eneo lisilo rasmi la uchimbaji madini ya dhahabu kusini magharibi mwa Burkina Faso, televisheni ya taifa iliripoti, wakiwakariri maafisa wa jimbo hilo.
Chanzo cha mlipuko huo katika jimbo la Poni bado hakijajulikana, kamishna mkuu wa Poni Antoine Douamba aliambia televisheni ya taifa.
Picha zilionyesha eneo kubwa la mlipuko wa miti iliyokatwa na kuharibu nyumba za bati. Miili iliyo saamba chini, imefunikwa kwa mikeka.
Haikuwa wazi ni aina gani hasa ya uchimbaji wa dhahabu ulifanyika kwenye eneo hilo. Burkina Faso kuna migodi mikubwa ya dhahabu inayoendeshwa na makampuni ya kimataifa, lakini pia kuna mamia ya maeneo madogo yasio rasmi ambayo yanafanya kazi bila uangalizi au udhibiti.