Polisi wameongeza kusema Ijumaa jioni kwamba walizuilia raia wanne wa Afghanistan, na wawili wa Uturuki, wanaoshukiwa kumiliki bunduki pamoja na vilipuzi kinyume cha sheria.
Haijabainika iwapo watafunguliwa mashitaka kutokana na ufyatuliaji huo wa risasi. Ghasia kati ya makundi ya wahamiaji zilizuka mapema Ijumaa kwenye ghala moja lililopo shambani, karibu na kijiji cha Horgos.
Polisi walifanya msako kwenye ghala hilo na kupata bunduki mbili za rashasha pamoja na risasi. Pia walipata wahamiaji 79 ambao walipelekwa kwenye vituo vya mapokezi, taarifa zimeongeza.
Ripoti za ghasia na vita vya bunduki zimeongezeka katika siku za karubi karibu na mpaka kati ya Serbia na Hungary.