Hilo limetokea siku chache baada ya serikali kusema kwamba hali ya utulivu ilikuwa imerejeshwa mkoani humo. Vikosi vya Amhara katika siku za karibuni vimekuwa vikikabiliana na jeshi la serikali wakati likijaribu kuvipokonya silaha, ambapo wiki iliyopota baadhi ya miji jimboni humo ilichukuliwa tena na serikali.
Wakati huo huo kwa mujibu wa shirika la habari la AP, Tume ya Haki za Binadamu iliyoteuliwa na serikali imesema Jumatatu kwamba kuna ripoti za kuaminika kwamba kumekuwa na mashambulizi kadhaa ya makombora kwenye mji wa Fenote Selam pamoja na mingine ya Amhara, ambayo yamepelekea raia kujeruhiwa.
Ripoti zimeongeza kwamba viongozi wa Amhara wanalengwa huku baadhi wakiuwawa, wakati miundombinu ikisambaratika kwenye maeneo mengi ya mkoa huo.