Washambuliaji hao walivamia eneo la Serikali ya Mtaa ya Zangon Kataf katika jimbo la Kaduna na kufyatua risasi Jumamosi baada ya makabiliano na polisi katika kituo cha ukaguzi, Yabo Ephraim, msemaji wa serikali ya eneo hilo aliambia shirika la habari la Associated Press.
Washambuliaji hao walivamia eneo la Zangon Kataf katika jimbo la Kaduna na kufyatua risasi Jumamosi baada ya makabiliano na polisi katika kituo cha ukaguzi, Yabo Ephraim, msemaji wa serikali ya eneo hilo aliambia The Associated Press.
Maafisa waliweka marufuku ya kutoka nje katika eneo hilo baada ya shambulio hilo.
Washambuliaji walikuwa wa kabila la Fulani, kundi la wafugaji wengi wa kuhamahama ambao wameingia katika mgogoro wa muda mrefu na wakulima kuhusu upatikanaji mdogo wa maji na ardhi, Ephraim alisema.
Kabla ya kurushiana risasi, mapigano yalikuwa yamezuka kati ya baadhi ya wanakijiji na kikundi kidogo cha wanaume wa kabila la Fulani. Waliondoka eneo la tukio na baadaye walirudi kwa wingi wakiwa na bunduki na mapanga, msemaji wa serikali alisema.