Watu 16 wafariki na karibu darzeni tatu kujeruhiwa katika ajali ya majengo Cameroon

Shugaban Kamaru, Paul Biya

Maafisa wanasema takriban watu 16 waliuwawa na karibu darzeni tatu kujeruhiwa siku ya Jumapili wakati jengo la ghorofa nne lilipoangukia kwenye jengo dogo katika jiji kubwa zaidi nchini Cameroon.

Idadi ya majeruhi inaweza kuwa kubwa zaidi alisema Samuel Dieudonne Ivaha Diboua gavana wa eneo la Littoral la Cameroon ambako Douala ipo.

Gavana huyo alisema kuwa waokoaji wakisaidiwa na wanajeshi wa serikali ya Cameroon bado wanachimba kwenye mabaki ili kuona kama miili zaidi inaweza kupatikana. Kikosi cha zima moto cha jeshi kimeamriwa kuungana na shirika la msalaba mwekundu nchini humo na huduma nyingine za uokoaji katika kutafuta walionusurika.