Your browser doesn’t support HTML5
Akitoa kauli hiyo ya serikali bungeni Dodoma Jumatatu waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania Dr.Emmanuel Nchimbi aliwasihi wananchi kuwa watulivu wakati serikali ikiwasaka wale waliofanya shambulio hilo.
Maafisa nchini Tanzania wamewakamata watu 10 ikiwa ni pamoja na raia wanne wa Saudia Arabia .
Shambulizi hilo lilitokea wakati kanisa hilo jipya lilipofanya misa yake ya uzinduzi iliyohudhuriwa na balozi wa Vatikan nchini Tanzania .
Mashahidi kutoka kwenye eneo la tukio wanasema guruneti lilirushwa kwenye umati wa watu karibu na mlango wa kuingilia kanisani.
Your browser doesn’t support HTML5
Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo ametangaza kukamatwa kwa watu hao siku ya jumatatu.
Hali katika hospitali ya Mount Meru Arusha ilikuwa tete huku madaktari wakifanya kila wawezalo kuhudumia idadi kubwa ya wagonjwa kwa wakati mmoja. Sauti ya Amerika ilizungumza na Daktari Haika Mhando wa Mount Meru na kutaka kujua hali hospitalini hapo.
Your browser doesn’t support HTML5