Mashirika mbali mbali duniani yamekuwa yakijitokeza kujaribu kuwasaidia wanawake ili waweze kujikimu kimaisha na pia kuibadilisha jamii inayowazunguka.
Mfano ni taasisi ya Umoja wa Mataifa (UN) ambapo Julai mwaka 2010, taasisi hiyo ilianzisha kitengo maalum kinachofahamika kama UN Women lengo likiwa ni kuangazia matatizo wanayopitia wanawake duniani na kisha kutafuta suluhu.
Huku juhudi zikiendelea, imebainika kwamba wanawake wanaoishi maeneo ya vijijini hasa barani Afrika wanakumbwa na matatizo mengi ikilinganishwa na wenzao wanaoishi mijini.
Your browser doesn’t support HTML5
Baadhi wa wanawake katika vijiji huko pwani ya Kenya wako mstari wa mbele katika kujishughulisha na shughuli mbali mbali za kuwaongezea kipato ili kujikimu kimaisha.