Wanamgambo wa ki-Houthi wanaoungwa mkono na Iran nchini Yemen wamedai kuhusika na shambulio la kombora siku ya Jumanne katika meli inayobeba kontena kwenye bahari ya Sham na kwa jaribio la kuishambulia Israel kwa kutumia ndege zisizokuwa na rubani.
Meli ya MSC Mediterranean Shipping imesema hakuna majeruhi kwa wafanyakazi wake kutokana na shambulio hilo katika meli yake, the United VIII ilikuwa ikisafiri kutoka Saudi Arabia kuelekea Pakistan. Ilisema meli hiyo iliiarifu meli ya kivita ya ushirika wa karibu kwamba imeshambuliwa na imechukua mbinu za kukwepa.
Israel imesema katika tukio tofauti, kuwa ndege yake ilizuia mashambulizi ya angani kwenye eneo la bahari ya Shamu. Msemaji wa jeshi la ki-Houthi, Yahya Sarea amesema katika hotuba yake kwa njia ya televisheni kuwa kundi hilo lili-ilenga meli hiyo, ambayo aliitaja kama MSC United, baada ya wafanyakazi hao kushindwa kujibu tahadhari.