Wizara ya ulinzi ya Russia ilisema Alhamisi mamia zaidi ya wanajeshi wa Ukraine wamejisalimisha katika kiwanda cha chuma cha Azo-vstal kilichozingirwa huko Mariupol, na kufanya jumla ya wiki hii kufikia 1,730.
Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu ICRC ilisema katika taarifa yake ilikuwa ikiwasajili wapiganaji walioondoka Azo-vstal, operesheni iliyoanza Jumanne na inaendelea Alhamisi.
Kamati hiyo ilisema haisafirishi wafungwa wa kivita hadi mahali ambapo wanashikiliwa, kundi hilo la misaada lilisema. Mchakato wa usajili unahusisha mtu binafsi kujaza fomu yenye maelezo binafsi kama vile jina, tarehe ya kuzaliwa na jamaa wa karibu. Taarifa hizi huruhusu Msalaba mwekundu kufuatilia wale ambao wametekwa na kuwasaidia kuwasiliana na familia zao.