Kamanda wa vikosi vya Ufaransa huko Sahel alisema Ijumaa kwamba wanajeshi 1,500 wa Ufaransa wataondoka Niger ifikapo Disemba 31 muda uliotangazwa na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron mwishoni mwa mwezi uliopita.
Uondokaji huo uliotakiwa na watawala wa kijeshi wa Niger ulianza wiki iliyopita baada ya kuondolewa kwa Rais Mohamed Bazoum mwezi Julai ambaye ni mshirika mkuu wa Paris ulipelekea mkakati wa Ufaransa kwa eneo la Sahel kuyumba.
“Lengo la matangazo ya Rais ya kuondoka ifikapo Disemba 31 litafikiwa” alisema Jenerali wa Ufaransa Eric Ozanne kwenye mkutano wa pamoja na waandishi wa habari akiwa na kanali wa Niger, Mamane Sani Kiaou katika mji mkuu Niamey.
Kanali huyo wa Niger aliongeza kuwa wanajeshi 282 tayari wameondoka nchini humo kufikia/kuanzia leo”.
“Misafara miwili mikubwa ya magari ya jeshi ambayo ilikuwa katika ukanda wa kaskazini” imeondoka alisema Ozanne akiongeza kuwa idadi kadhaa ya misafara iliyobeba vifaa visivyokuwa na mashaka ilianza kuondoka kwenye eneo.
Alisema msafara huu haukujumuisha vifaa vya silaha au mawasiliano.
Mtiririko mkubwa wa msafara wa vifaa utaanza wiki ijayo aliongeza kwamba makontena 2,500 yapo tayari kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi.
“Kazi hii imekuwa ikifanywa na makundi ya raia kutoka nje na kwa uwazi kabisa hasa kwa wakaazi wa eneo hilo ambao watashuhudia malori pekee yenye makontena”, alisema.