Wanajeshi wa Russia wateka kinu cha nyuklia -Maafisa wa Ukraine

Watu wanaokimbia kutoka Ukraine wakipanga foleni ya kupanda basi kwenye kivuko cha mpaka huko Medyka, Poland, Ijumaa, Machi 4, 2022. Zaidi ya watu milioni 1 wameikimbia Ukraine kufuatia uvamizi wa Russia. (Picha ya AP/Markus Schreiber)

Rais wa Marekani Joe Biden alizungumza na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy na kupokea taarifa kuhusu moto katika kinu hicho.

Maafisa wa Ukraine wanasema kuwa wanajeshi wa Russia wamechukua udhibiti wa kinu kikubwa zaidi cha nyuklia barani Ulaya, Zapori-zhzhia, karibu na mji wa Ener-hodar wa Ukraine, baada ya kukishambulia kwa makombora na kusababisha moto katika jengo katika eneo la mtambo huo.

Wakaguzi wa nyuklia wa Ukraine walisema hapakuwa na uvujaji wa mionzi kwenye kiwanda hicho na kuongeza kuwa wafanyakazi wa kiwanda wanaendelea kufanya kazi kwa usalama. Maafisa wa Ukraine walisema wazima moto waliweza kudhibiti moto huo katika kituo hicho.

Viongozi wa nchi za magharibi na watetezi mazingira wamelaani shambulio hilo na uingereza kutoa wito wa kuitisha kikao cha dharura cha baraza la usalama kuzungumzia suala hilo.

Ener-hodar ni jiji muhimu la kuzalisha nguvu umeme kwenye Mto Dnieper karibu kilomita 700 kusini mashariki mwa Kyiv. Kituo kinazalisha karibu asilimia 25 ya nishati ya Ukraine.

Rais wa Marekani Joe Biden alizungumza na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy na kupokea taarifa kuhusu moto katika kinu hicho, kulingana na taarifa ya White House iliyotolewa jana Alhamisi.

Taarifa kutoka kwa Shalanda Young, kaimu mkurugenzi wa Ofisi ya Rais, imesema kwamba utawala wa Biden umeomba msaada wa ziada wa dola bilioni 10 kutoka bungeni ili kugharimia huduma za dharura, usalama, na kiuchumi nchini Ukraine na nchi jirani katika siku na wiki zijazo, ilisema. Usimamizi na Bajeti. Pesa hizo, alisema, zitagharamia vifaa vya ulinzi, msaada wa dharura wa chakula, kupelekwa kwa wanajeshi wa Marekani katika nchi jirani na utekelezaji wa vikwazo wenye nguvu zaidi.