Wanaharakati wa LQBTQ Nigeria walalamikia kuendelea kushikiliwa kwa wanandoa waliokamatwa Jumatatu

Naibu waziri mkuu wa Canada Chrystia Freeland akiwa kwenye maandamano ya kuunga mkono jamii ya LGBTQ mjini Toronto, Ontario, Canada. Juni 25 , 2023.

Wanaharakati wa haki za wapenzi wa jinsia moja nchini Nigeria wamelalamikia kukamatwa na kuzuiliwa wiki hii kwa darzeni ya watu waliohudhuria harusi ya wapenzi wa jinsia moja hapo Jumatatu.

Ukamataji huo umetajwa kuwa mkubwa zaidi katika miaka ya karibuni dhidi ya jamii ya LQBTQ nchini humo. Msemaji wa polisi wa Nigeria amesema kwamba watu 67 wameendelea kushikiliwa kwa tuhuma za kuhudhuria harusi ya wapenzi wa jinsia moja kwenye mji wa jimbo la Delta wa Ekpan.

Polisi wa jimbo hilo wamesema kwamba walipata taarifa kuhusu harusi hiyo baada ya kuhoji mmoja wa wageni walioalikwa Jumapili, wakati walipokuwa wakipiga doria. Haijabainika iwapo mtu huyo alihojiwa kutokana na mavazi yake.

Kutokana na ripoti walizokusanya, polisi walivamia harusi hiyo Jumatatu, na kukamata wanandoa pamoja na wageni walioalikwa. Mamlaka zilionyesha waliokamatwa kwa wanahabari zikisema kwamba watawajibishwa kisheria.

Msemaji wa polisi wa Delta Bright Edafe, ameambia VOA kwa njia ya simu kwamba wamepata idhidi ya mahakama ya kuendelea kuwashikilia watu hao, wakati wakikusanya ushahidi zaidi.