Hata baadhi ya wanafunzi ambao wamepata chanjo, na baadhi wanaotaka wapatiwe chanjo, wanapinga sera hiyo na umoja wa wanafunzi unatishia kuitisha maandamano ya nchi nzima.
Vyuo vikuu kote nchini Afrika Kusini vinajiweka sawa kwa mwaka mpya wa masomo wakati nchi ikiibuka kutoka katika wimbi la nne la janga la virusi vya corona.
Chanjo za kuzuia Covid 19 zitakuwa ni lazima kwa wengi kurejea kwenye majengo ya vyuo.
Umoja wa wanafunzi Afrika Kusini umeonya kuwa maandamano dhidi ya amri ya chanjo yanatarajiwa kufanyika.
Katika chuo kikuu cha Johannesburg, wanafunzi wanasema wamekasirishwa kwamba hawakushauriwa, wanadai kuwa sera zinaingilia kati haki zao za kikatiba kuhusu uadilifu wa kimwili.
Mxolisi Manana ni rais wa baraza la wanafunzi katika chuo kikuu cha Johannesburg, anasema “wanafunzi lazima waende kupata chanjo kwa ridhaa yao,. Kwahiyo, iwapo hawajapatiwa chanjo au wamepatiwa, wakati watakapoondoka kwenye maeneo ya chuo kwenda kufanya manunuzi madukani au wakienda sehemu yoyote, wanaweza kukutana na watu ambao wamechanjwa au ambao hawajachanjwa.”
Chini ya nusu ya watu wazima nchini Afrika Kusini wamepatiwa chanjo na hakuna amri ya kitaifa kuhusu chanjo.
Sababu zinazohusisha na kusita kupatiwa chanjo zina mkanganyiko.
Wanafunzi wanasema uamuzi wao ulifanywa kwa sababu binafsi, tamaduni na imani za kidini, licha ya kuwa hakuna ushahidi kama mbinu hizo zinawalinda dhidi ya Covid 19.
Hlengwe Xulu ini mwanafunzi mahiti katika chuo kikuu cha Johannesburg, anasema “kuanzia wimbi la kwanza nimekuwa nikitumia matibabu ya kienyeji ya kiafrika. Sijalazwa hospitali. Sijawahi kukutwa bna Covid. Nadhani kwa sababu hiyo imenisaidia mpaka hivi sasa, nitaendelea kutumia tiba za nyumbani. Watu ambao wamepatia chanjo wanasemekana kulindwa na virusi na pengine ni rahisi kwao. Wasiwa na wasi wasi na ukweli kwamba kuna mtu mmoja anachagua kutopatiwa chanjo ambaye anatumia haki yake ya msingi.”
Chanjo zinawalinda watu, hasa dhidi ya kuumwa sana. Lakini mmoja wa madaktari wa juu nchini humo anasema wale ambaohawakupatiwa chanjo nao ni hatari katika kupata au kusambaza Covid 19. Dr. Shabur Madhi profesa wa masuala ya chanjo katika chuo kikuu Witwatersrand anaelezea zaidi.
“Wako katika hali ya kuishia hospitali, katika chumba cha watu mahututi ICU na kufariki kwa Covid 19. Kuishia hospitali siyo tu mzigo ambao kila mtu ataubeba. Ni mzigo ambao watashirikiana katika jamii nzima, wote katika misingi ya ufadhili wa mfumo wa huduma za afya, pamoja na matokeo mengine ambayo yatajitokeza hospitali ambapo kuna haja kupunguza, kwa mfano, upasuaji kwasaabu vituo vya huduma za afya viko katika shinikizo,” anasema.
Ndiyo maana anataka hatua kali sana kwa wale ambao wanasita kupatiwa chanjo, “Maamuzi yote yana matokea yake. Ndyo sababu ya msngi, kuwepo kwa amri ya kupata chanjo hakuna maana kwamba tutakulazimisha au kukuweka gerezani kama ukichagua kutochanja.”
“Kwa wanafunzi ambao hawakupokea chanjo, watapoteza fursa ya kuwepo kwenye majengo ya chuo kikuu.
Kikuu cha Johannesburg kimesema katika taarifa yake kuwa misamaha itatolewa na kufikiriwa katika misingi ya afya au kidini. Wanafunzi watakaopewa msamaha watakuwa wanapimwa Covid kila wiki.