Chombo cha habari cha serikali ya Iran kimesema kwamba wasichana 20 wa shule wamelazwa hospitali Jumanne, ikiwa tukio la karibuni la wimbi la mashambuizi ya ajabu ya kuwekewa sumu, na kuwaathiri maelfu ya wanafunzi katika siku za karibuni.
Ripoti zimeongeza kusema kwamba wanafunzi hao walipokea matibabu baada ya kukumbwa na matatizo ya kupumua kwenye mji mkuu wa jimbo la kaskazini magharibi la East Azerbaijan, wa Tabriz, kwa mijibu wa shirika hilo la habari la IFRNA.
Ukionekana kuwa msururu wa matukio, tangu Novemba mwaka jana, zaidi ya wanafuzi 5,000 wameathihiwa na kuzirai, kutapika na kushindwa kupumua miongoni mwa dalili nyingine, baada ya kudai kunusa harufu isiyopendeza, huku baadhi wakilazimika kupelekwa hospitali.
Mshambulizi hayo ambayo bado hayajabainika kwenye takriban shule 230, yamezua hofu pamoja na ghadhabu miongoni mwa wanafunzi na wazazi wao.