Wamarekani wameanza maadhimisho ya Martin Luther King Jr

Mwaka 1963, Martin Luther King, Jr. alitoa hotuba yake maarufu ya “I Have a Dream Speech” wakati wa maandamano yanayohusu ajira na uhuru kwenye eneo la Lincoln Memorial

Chini ya kauli mbiu ya "It Starts With Me". kizazi cha King kinatarajia kuchochea maendeleo kwa kuwasaidia Wamarekani zaidi kuelezea mapambano yanayoendelea ya usawa wa rangi na maelewano

Heshima na maadhimisho ya kila mwaka ya maisha na urithi wa Mchungaji Martin Luther King Jr ambayo huanza nchi nzima Ijumaa kwa kawaida hujumuisha matukio mchanganyiko katika siasa, imani na huduma za jamii.

Kwa sherehe za mwaka huu za 37 tangu kutambuliwa kwake katika serikali kuu mwaka 1986 kizazi cha King kinatarajia kuchochea maendeleo kwa kuwasaidia Wamarekani zaidi kuelezea mapambano yanayoendelea ya usawa wa rangi na maelewano. Bernice King, binti wa marehemu King kinara wa haki za kiraia alisema watu lazima wawe juu zaidi kujitambua katika kuimarisha ahadi zao wenyewe kwa maendeleo yanayohitajika.

"Tunahitaji kubadilisha mawazo yetu," alisema King ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha King huko Atlanta.

Chini ya kauli mbiu ya "It Starts With Me", kituo hicho kilizindua hafla zake za Siku ya Martin Luther King Jr siku ya Alhamisi kwa mikutano ya vijana na watu wazima ili kuuelimisha umma juu ya njia za kubadilisha mifumo isiyo ya haki nchini Marekani.

Mikutano hiyo ilitangazwa kwenye mitandao na inapatikana pia kwenye akaunti za mitandao ya kijamii ya kituo hicho.