Wakimbizi wanyanyaswa katika kambi za Afrika Mashariki

Hali mbaya kwa wakimbizi katika kambi ya IFO 1 huko Dadaab, karibu na mpaka wa Kenya na Somalia.

Kenya hivi karibuni iliwaamrisha wakimbizi wote walohama katika miji mbali mbali kurudi katika kambi ya Dadaab, kambi kuu ya wakimbizi barani Afrika, hiyo ikiwa njia moja ya kujibu wimbi la masham bulizi ya kigaidi katika miji ya nchi hiyo.

wakimbizi wanaeleza kwamba wanalazimika kuhama kambi kutokana na ukosefu wa huduma msingi, unyanyasaji, uhalifu, ubakaji na hakuna mfumo wa elimu kwa watoto wanaoishi kwa muda mwingi ndani ya kambi.

Your browser doesn’t support HTML5

Wakimbizi wanyanyaswa Afrika Mashariki


Katika mjadala kwenye kipindi cha :"Live Talk", cha Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika, wakimbizi na wanaharakati wa kutetea haki zao wanadai hali ianweza kuwa mbaya hasa kutokana na unyanyasaji, uhalifu na ubakaji katika kambi nyingi za Afrika Mashariki.

Wakimbizi wanatoa wito kwa serikali kuheshimu makubaliano ya kimataifa juu ya wakimbizi na kudai wamechoka kukimbia unyanyashaji na ghasia wanahitaji amani na utulivu kama raia wengine.