Wakati saa ilipogonga saa sita usiku katika mji mkubwa kabisa wa Austrialia, tani ya vilipuzi vilizuka katika maonyesho ya muda wa dakika 12 ambavyo vililenga kwenye Sydney Harbour Bridge. Zaidi ya waztu milioni moja, idadi ambayo ni moja ya tano ya wakazi wa mji humo, iliangalia kutoka kwenye fukwe na kutoka kwenye boti zilizokuwepo bandarini.
“Ilikuwa ni ukichaa,” alisema mtalii wa kijerumani Janna Thomas, ambaye alitembea kwenye mstari tangu saa moja na nusu asubuhi, ili kuweza kupata nafasi nzuri mbele ya ufukwe wa bahari katika eneo la Sydney Botanic Garden. “Si rahisi kupata sehemu nzuri ya kukaa, lakini mandhari yake yalikuwa mazuri sana.”Aliongeza kusema.
Huko Auckland, mvua nyepesi iliyokuwa inanyesha iliisafisha anga saa sita usiku ilipofika, huku watu milioni 1.7 wa mjini humo wakianza kuhesabu huku taa za rangi rangi zikiipaba hewa kati na jengo hilo lenye urefu wa futi 1,076, la mawasiliano likiwa ndiyo kivutio kikuu.
Licha ya yote hayo ya kuukaribisha mwaka mpya, huko Ukraine na Gaza vita vilikuwa vinaendelea na mivutano ilizidi kuongezeka katika sehemu nyingine za dunia, na kuathiri sherehe za mkesha wa mwaka mpya, na baadhi ya sherehe za mkesha wa mwaka mpya zikifutwa kabisa kwenye baadhi ya maeneo.