Wakaazi nchini Botswana wameandamana kupinga mswaada wa kuhalalisha ushoga

Jamii ya mashoga (LGBTQ) wakisheherekea maamuzi ya mahakama kuu Zimbabwe 2019 kuunga mkono haki za LGBTQ. Gaborone, Botswana.

Maandamano hayo yaliyoungwa mkono na makundi ya kidini, yalifanyika mji mzima kuelezea upinzani wao kwa mswaada ambao una lengo la kutekeleza maamuzi ya mahakama mwaka 2019 yanayounga mkono haki za LGBTQ

Mamia ya watu waliingia mitaani katika mji mkuu wa Gaborone nchini Botswana siku ya Jumamosi kupinga dhidi ya mswaada unaotaka kuhalalisha mahusiano ya jinsia moja.

Maandamano hayo yaliyoungwa mkono na makundi ya kidini, yalifanyika mji mzima kuelezea upinzani wao kwa mswaada ambao una lengo la kutekeleza maamuzi ya mahakama mwaka 2019 yanayounga mkono haki za LGBTQ.

Baadhi walishika mabango yanayosomeka “Tunasema hapana kwa ushoga” na “Tuwalinde watoto wetu”. Mswaada huo utafungua milango ya uasherati na upotoshaji alisema mchungaji Pulafela Mabiletswane Siele wa ushirika wa ki-Injili wa Botswana, kundi la dhehebu la kikristo wakati akisoma ombi kwenda kwa wabunge. "Tunalisihi bunge letu lichague kura ya maoni kuhusu suala hili", alisema Siele.

Maandamano hayo yanafanyika wakati kuna shinikizo kubwa dhidi ya haki za LGBTQ huko kusini mwa Afrika.