Wajumbe wa Repablikan wa Marekani wakutana kutadhimini mikakati ya kupata Spika mpya

Mwakilishi Jim Jordan kutoka Ohio, mmoja wa wagombea wa uspika wa baraza la wawakilishi la Marekani.

Warepablikan kwenye baraza la wawakilishi la Marekani Jumatano wamekutana, ili kuanza kikao cha faragha cha upigaji kura ikiwa hatua ya kukubaliana kuhusu atakayekuwa spika mpya.

Wagombea wawili wanaoongoza, ambao ni wawakilishi Jim Jordan, na Steve Scalise Jumanne wamewahutubia wanachama wa chama chao wakieleza ni kwa nini wanahitaji kupewa wadhifa huo, ulioachwa wazi baada ya kuondolewa kwa spika Kevin McCathy wiki iliyopita.

McCathy tarayi amewaambia wenzake kwamba wasimteue kuchukua nafasi hiyo tena. Warepablikan wana wingi mdogo wa wajumbe 221 dhidi ya wademokrat 212 kwenye baraza hilo, ikiwa na maana kwamba watahitaji uungaji mkono wa wote ili kupata wingi mdogo unaohitajika katika kumpata spika.

McCathy alipigiwa kura mara 15 kabla ya kupata ushindi hapo Januari kutokana na kuwa wademokrat kuungana pamoja nyuma ya mgombea wao, ambaye ni kiongozi wao sasa mwakilishi Hakeem Jeffries, wakati baadhi ya Warepabalikan wakisusia kumpigia kura McCathy hadi dakika za mwisho.