Wajumbe wa China, Iran na Pakistan wamekutana kwa mara ya kwanza kwa mazungumzo ya pande tatu dhidi ya ugaidi na usalama wa kikanda siku ya Jumatano mjini Beijing.
Wajumbe walifanya majadiliano ya kina juu ya hali ya usalama wa kikanda, hasa tishio la ugaidi linalokabiliwa na kanda hiyo, ilisema taarifa ya baada ya mkutano huko Islamabad, ambayo haikutoa maelezo zaidi. Wizara za mambo ya nje za Pakistan na China zimesema mataifa hayo matatu yameamua na kufanya mkutano huo kua jambo la kawaida na kufanyika mara kwa mara.
Maafisa waandamizi wa kupambana na ugaidi kutoka China, Pakistan na Iran, kila mmoja kutoka wizara zao za kigeni, waliongoza timu zao katika mazungumzo ya Jumatano. Wachambuzi wanasema jimbo la kusini magharibi mwa Pakistan la Baluchistan huenda lilikuwa ajenda muhimu. Eneo lenye utajiri wa mali-asili lakini maskini ni sehemu muhimu kwa mpango wa mabilioni ya dola unaofadhiliwa na China, njia muhimu ya Uchumi wa China na Pakistan.
Kuanzishwa kwa utaratibu wa usalama wa pande tatu kati ya China, Pakistan na Iran kunaonyesha wasiwasi wao wa pamoja kuhusu usalama katika Baluchistan, alisema Baqir Sajjad, wa Pakistan kutoka Kituo cha Wilson cha mjini Washington. Sajjad alisema hali ya uthabiti katika Baluchistan ni muhimu kwa mafanikio ya kutekeleza miradi ya CPEC huko.