DRC yatangaza wagonjwa wa mwisho wa Ebola

mtoto akipatiwa chanjo ya ebola DRC.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilitoa wagonjwa wake wa mwisho wa Ebola waliothibitishwa kutoka vituo vya matibabu siku ya Jumatatu, maafisa wa afya walisema, na kuanza kuhesabu siku 42 za kutangaza nchi hiyo haina virusi.

Kuruhusiwa kwa wagonjwa sita siku ya Jumatatu kutoka kwenye vituo vya matibabu katika mkoa wa Kivu Kaskazini kunaweza kuashiria mwisho wa mwezi mzima wa kurudi kwa janga la mwaka 2018-20, la Ebola ambalo liliua watu zaidi ya 2,200 kabla ya kutangazwa kumalizika mwezi Juni 2020.

Kesi kumi na mbili zimeripotiwa tangu virusi kuibuka tena mwanzoni mwa Februari, na kuua watu sita. Ni wiki tatu zimepita tangu maafisa wa afya wa Kivu Kaskazini kugundua kesi mpya.