Wafungwa hao walirushiana risasi na walinzi wa magereza wakati wakitoroka jumapili usiku, na kuwauwa walinzi wawili na kuwajeruhi wawili, kulingana na wizara ya mambo ya ndani ya Mauritania
Wafungwa wanne wanajihadi wametoroka katika gereza moja huko Nouakchott, mji mkuu wa Mauritania.
Wafungwa hao walirushiana risasi na walinzi wa magereza wakati wakitoroka jumapili usiku, na kuwauwa walinzi wawili na kuwajeruhi wawili, kulingana na wizara ya mambo ya ndani ya Mauritania.
"kikosi cha ulinzi wa Taifa kimeimarisha udhibiti wake katika gereza hilo na mara moja kilianza kuwafuatilia watoro hao ili kuwakamata haraka iwezekanavyo," wizara hiyo ilisema katika taarifa jumatatu.
Wafungwa wawili walikuwa wamehukumiwa kifo na wengine wawili walikuwa wakisubiri kesi kwa mashtaka ya kuwa wanachama wa kundi la kigaidi, kulingana na shirika la habari la Agence France Presse.