Wafuasi wa Rais Mnangagwa nchini Zimbabwe wanajiandaa kwa uchaguzi

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akizungumza na wanachama wa ZANU-PF mjini Harare

Rais Emmerson Mnangagwa katika mkutano wake wa hivi karibuni aliwaambia wanawake nchini humo kwamba wao ni kiungo muhimu kwa chama cha ZANU-PF na kura zao ni muhimu kwa ajili ya ushindi wa chama hicho

Katika ukumbi mkubwa kwenye makao makuu ya chama tawala cha Zimbabwe cha ZANU-PF wanawake waliitikia kwa shangwe kubwa wakati Rais Emmerson Mnangagwa alipowaelezea kuwa wao ni kiungo kikuu wa chama hicho ambapo kura zao ni muhimu kwa ajili ya ushindi katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Agosti.

Katika mkutano wa hivi karibuni wa upinzani, wanawake wakiwa wamevalia nguo zenye picha ya sura ya kiongozi wao wa kiume wa chama hicho, waliimba, wakicheza na kuahidi kupiga kura kwa ajili ya mabadiliko, kamwe hawajali kwamba uchaguzi huo unawakilisha tena hali ambapo wanawake kwa kiasi kikubwa wanakuwa ni washangiliaji tu.

Hali inaonekana kuwa mbaya zaidi mwaka huu kwa sababu idadi ya wagombea wanawake imepungua, licha ya wanawake kuwa na idadi kubwa nchini humo, na kwa kawaida, ndio idadi kubwa ya wapiga kura.