Kampuni ya Empire Navigation, inayoimiliki imesema kupitia taarifa kwamba mshirika wake amewasiliana na mamlaka za Iran, na kuripoti kwamba wafanyakazi wote waliokuwa kwenye meli hiyo kwa jina St Nikolas, wapo salama na wenye buheri ya afya.
Kampuni hiyo imeongeza kwamba haijaweza kuwasiliana moja kwa moja na wafanyakazi wote 19 wa meli hiyo iliyopeperusha bendera ya visiwa vya Marshall, na kulazimishwa na Iran kutia nanga kwenye bandari ya Bandar Abbas.
Miongoni mwa wafanyakazi hao,18 ni raia wa Ufilipino, na mmoja raia wa Ugiriki. Iran ilisema kwamba ilikamata meli hiyo karibu na Oman Alhamisi, kulalamikia wizi wa mafuta yake kutoka kwenye meli hiyo na Marekani mwaka jana, wakati huo ikijulikana kama Suez Rajan, chombo cha habari cha serikali kimesema.