Waasi wa kundi la ADF wamekuwa wakifanya operesheni zao tangu kati-kati ya miaka ya 1990 mashariki mwa DRC, ambako wamewaua maelfu ya raia. Mwaka 2019 waliahidi kulitii kundi la Islamic State, ambalo linasema ADF ni mshirika wake Jamhuri ya Afrika ya kati.
Takriban wanachama 200 waasi wa ADF wenye uhusiano na kundi la Islamic State waliuawa katika mashambulizi ya anga yaliyoongozwa na Uganda mwezi Septemba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, rais wa Uganda amesema.
Waasi wa kundi la ADF wamekuwa wakifanya operesheni zao tangu kati-kati ya miaka ya 1990 mashariki mwa DRC, ambako wamewaua maelfu ya raia. Mwaka 2019 waliahidi kulitii kundi la Islamic State, ambalo linasema ADF ni mshirika wake Jamhuri ya Afrika ya kati.
Tumekuwa tukifanya mashambulizi ya anga dhidi ya magaidi nchini Congo”, Rais Museveni alisema katika mtandao wa X, zamani Twitter, kabla ya kudai kuwa karibu waasi 200 kati yao waliuawa katika mashambulizi yaliyofanywa Septemba 16.