Wa-Comoro walipiga kura katika uchaguzi wa rais siku ya Jumapili, huku rais wa sasa Azali Assoumani akisema ana imani kupata ushindi wakati upinzani unadai kulikuwa na udanganyifu katika uchaguzi.
Viongozi kadhaa wa upinzani katika visiwa vya Bahari ya Hindi walikuwa wamewataka wapiga kura kususia uchaguzi huo, ambapo wagombea watano wamejitokeza dhidi ya Assoumani mwenye umri wa miaka 65 kushika nafasi hiyo ya juu. “Nina imani kwamba nitashinda duru ya kwanza.
Ni Mwenyenzi mungu ambaye ataamua na watu wa Comoro,” rais alisema baada ya kupiga kura katika mji wake wa Mitsoudje, nje kidogo ya mji mkuu Moroni. “Kama nitashinda duru ya kwanza, itaokoa muda na pesa,” aliongeza.
Lakini wagombea wa upinzani walishutumu “udanganyifu” na “masanduku kujaa kura ” katika maeneo kadhaa, baada ya upigaji kura kuanza kwa kuchelewa.