Vyombo vya usalama Russia vilipitia kipindi cha mkanganyiko; Inasema Uingereza

Mfano wa vifaa vya kijeshi vya kundi la mamluki la Wagner la Russia

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema Jumapili katika taarifa yake ya kila siku ya ujasusi kuhusu uvamizi wa Russia nchini Ukraine. Hivi sasa hata hivyo mpango wa muda kwa mustakabali wa kikundi cha mamluki unajiweka vizuri, kulingana na ripoti iliyochapishwa kwenye Twitter

Vyombo vya usalama vya Russia vilipitia “kipindi cha mkanganyiko na mashauriano,” kufuatia uasi wa kundi la Wagner mwezi uliopita, Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema Jumapili katika taarifa yake ya kila siku ya ujasusi kuhusu uvamizi wa Russia nchini Ukraine.

Hivi sasa, hata hivyo mpango wa muda kwa mustakabali wa kikundi cha mamluki unajiweka vizuri, kulingana na ripoti iliyochapishwa kwenye Twitter. Wakati huo huo, baadhi ya makundi ya habari ya mitandao ya kijamii yanayohusishwa na Wagner yalianzisha tena matangazo yao, yakiangazia shughuli za Wagner barani Afrika.

Wizara hiyo imesema matangazo ya hivi karibuni kutoka kwa maafisa wa Russia yanaonyesha kuwa Russia “iko tayari” kukubali “matarajio ya Wagner ya kudumisha uwepo wake mkubwa katika bara hilo.”