Vurugu zazuka katika mkutano wa Bunge la Umoja wa Afrika

Your browser doesn’t support HTML5

Kulikuwa na vurugu katika mkutano wa Bunge la Umoja wa Afrika Jumatatu wakati wabunge walipokuwa wanagombania sanduku la kura na mwanamme mmoja alionekana amemlenga  kumpiga teke mbunge mwenzake wa kike huku kukiwa na kelele kuna watu wana silaha za moto ndani ya ukumbi.

Ugomvi mbalimbali ulitokea katika ukumbi wa mkutano huko Midrand, Afrika Kusini, wakati kutoelewana kulitokana juu ya mchakato wa kumchagua rais mpya kwa ajili ya baraza la kutunga sheria la AU

Shirika la utangazaji la taifa la Afrika Kusini, SABC, lilirusha matukio hayo.

Uchaguzi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika uliahirishwa wakati viongozi wakitafuta ufumbuzi wa kusonga mbele

Uchaguzi huo tayari uliaharishwa Alhamisi iliyopita pale mfanyakazi mmoja aliyekuwa anayefanya kazi karibu ofisi hiyo mjini Johannesburg aligundulika ana maambukizi ya virusi vya Corona.

Lakini mkutano huo wiki iliyopita kwa mara ya kwanza ulibaini mivutano wakati mbunge wa Afrika Kusini Julius Malema aliposikika akimtishia mbunge wa Mali Ali Kone katikati ya kikao hicho.

“Ntakuua tukitoka nje. Nje ya chumba hiki, Nitakuua. Nitakuua, “Malema, kiongozi machachari mropokaji wa chama cha upinzani cha mrengo wa kushoto zaidi nchini Afrika Kusini, alisikika akisema huku akimnyooshea kidole Kone.

Haya yote yanatokana na kutokubaliana kati ya kundi la nchi kutoka Afrika Magharibi na zile za Kusini mwa Afrika iwapo uongozi wa urais uhamishwe katika maeneo mbalimbali ya Afrika kwa utaratibu wa kuongoza kwa awamu katika nafasi hiyo.

Marais wawili wa Bunge la Umoja wa Nchi za Kiafrika wamekuwa wakitokea Afrika Magharibi na hapajawahi kuwa na rais kutoka kusini katika historia fupi ya bunge hilo, lililoanzishwa 2004.

Video hii ni kwa hisani ya PAN-AFRICAN PARLIAMENT