Volodymyr Zelenskyy ametoa hotuba kuwakumbuka watoto waliokufa Ukraine

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy

Zelenskyy amesema watoto 485 wamepoteza maisha kutokana na mashambulizi ya Russia. Hii ni idadi ambayo anasema wanaweza kuthibitisha rasmi, wakifahamu takwimu za kila mtoto. Idadi halisi ni kubwa zaidi, alisema.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alitumia hotuba yake ya kila usiku Jumapili kuwakumbuka watoto waliokufa kutokana na uvamizi wa Russia tangu mwaka 2014 akiwemo mtoto msichana wa miaka miwili aliyekufa katika mkoa wa Dnipro Jumamosi jioni.

Zelensky alisema kwamba Leo katika nchi yao ni siku ya kumbukumbu kwa watoto waliokufa kutokana na uvamizi wa Russia tangu mwaka 2014. Aliongeza kusema kua Watoto ambao wangekuwa hai hii leo kama kundi la majambazi katika Kremlin huko Moscow wasingejiona wakuu ambao wanadaiwa kuwa na haki ya kuamua hatima ya mataifa.

Zelenskyy amesema watoto 485 wamepoteza maisha kutokana na mashambulizi ya Russia. Hii ni idadi ambayo anasema wanaweza kuthibitisha rasmi, wakifahamu takwimu za kila mtoto. Idadi halisi ni kubwa zaidi, alisema. Pia alitaja watoto 19,505 wa Ukraine ambao walisafirishwa hadi Russia na bado wako katika mikono ya adui.