Vikosi vya usalama Nigeria vimewaokoa mateka kwenye kituo cha treni

Mfano wa vikosi vya usalama huko nchini Nigeria. March 3, 2021

Utekaji nyara wa kituo cha treni uliangazia kuenea kwa ukosefu wa usalama nchini Nigeria ambalo pia litakuwa suala kubwa kwa wapiga kura katika uchaguzi wa mwezi ujao kuchukua nafasi ya Rais Muhammadu Buhari

Vikosi vya usalama vya Nigeria vimewaokoa mateka wawili wa mwisho kutoka kwa utekaji nyara uliofanyika kwenye kituo cha treni kinachofahamika kuwateka na kuwakamata watu saba wakiwemo viongozi wawili wa vijiji maafisa walisema wiki hii.

Katika tukio la karibuni la utekaji nyara nchini Nigeria, watu wenye silaha walishambulia kituo cha treni cha vijijini, kusini mwa jimbo la Edo mapema mwezi huu, na kuwateka nyara darzeni ya abiria.

Utekaji nyara wa kituo cha treni uliangazia kuenea kwa ukosefu wa usalama nchini Nigeria ambalo litakuwa suala kubwa kwa wapiga kura katika uchaguzi wa mwezi ujao kuchukua nafasi ya Rais Muhammadu Buhari.

Kamishna wa mawasiliano wa jimbo la Edo, Chris Nehikhare amesema katika taarifa siku ya Jumatano kwamba mateka wawili wa mwisho wameokolewa na watu saba kuzuiliwa.

Wawili kati ya hao walikuwa machifu wa jadi wa eneo hilo.