Vikosi vya usalama vya Iran vililenga hospitali na bweni la wanafunzi usiku wa kuamkia Jumamosi, kundi la kutetea haki limesema leo, wakati vuguvugu la maandamano lililozuka kufuatia kifo cha Mahsa Amini likiingia wiki ya saba.
Amini, raia wa Iran mwenye umri wa miaka 22 mwenye asili ya Kikurdi, alifariki akiwa chini ya ulinzi baada ya kukamatwa mjini Tehran kwa madai ya kukiuka kanuni kali za mavazi ya Iran kwa wanawake kulingana na sheria ya Kiislamu.
Vikosi vya usalama vimejitahidi kudhibiti maandamano yanayoongozwa na wanawake ambayo yamebadilika na kuwa kampeni pana ya kuimaliza jamhuri ya Kiislamu iliyoanzishwa mwaka 1979.
"Kifo kwa dikteta," waombolezaji waliimba Jumamosi katika sherehe ya kuadhimisha siku 40 tangu kuuawa kwa muandamanaji katika mji wa magharibi wa Divandarreh, wakitumia kauli mbiu inayomlenga kiongozi mkuu Ayatollah Ali Khamenei.
Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema polisi wa kupambana na ghasia walimpiga risasi Mohsen Mohammadi, mwenye umri wa miaka 28, wakati wa maandamano huko Divandarreh hapo Septemba 19, na alifariki siku iliyofuata katika hospitali ya Kausar katika mji wa magharibi wa Sanandaj.
Dazeni ya watu ambao walikusanyika nje ya hospitali hiyo Ijumaa jioni kumlinda muandamanaji mwingine ambaye alishambulizi majeshi ya usalama, kundi la kutetea haki la Henaw lilisema.
“Watu alikusanyika mbele ya hospitali ya Kausar Sanandaj kumlinda Ashkan Mrwati ambaye alipigwa risasi na majeshi kandamizi,” ilisema taasisi hiyo yenye makao ya nchini Norway.
“Majeshi ya usalama yalimkamata Ashkan Mrwati wakai akiwa amejeruhiwa” ilisema taasis, kabla ya kutweet picha iliyosema ni yeye akiwa amelala kwenye kitanda cha kubebea wagonjwa na kuongea na wafanyakazi wa afya.
Wanafunzi waanzisha maandamano
Mara tu baada ya Hengaw kusema, majeshi hayo hayo ya usalama pia “yalifyatua risasi katika bweni la karibu la wanafunzi” katika chuo kikuu cha Afya cha Kikurdi.
Katika picha iliyowekwa kwenye mtandao na AFP, majeshi ya usalam yalionekana kuwasili hapo yakiwa katika zaidi ya darzeni za piki piki kabla ya kufyatua risasi kwenye jengo la bweni hilo.
Katika picha nyingine, majeshi ya usalama yalionekana kufyatua gesi ya kutoa machozi Ijumaa jioni kwenye makazi ya watu mjini Tehran katika ujirani wa Chitgar ambako maandamano makubwa yalikuwa yalifanyika usiku.
Wanafunzi walianzisha tena maandamano Jumamosi kwenye vyuo vikuu katika mji mkuu wa Tehran, Kreman kusini mwa Iran na mji wa magharibi wa Kermanshah miongoni mwa mingine, kwenye kanda ya video ambayo imesambaa sana kwenye mitandao ya kijamii.
Wanafunzi wa kike walikuwa wakipiga kelele kwenye mitaa ya Kermanshah nyakati za asubuhi kabla ya kuvamiwa na majeshi ya usalama, baadhi yao walijeruhiwa, wakiwemo wawili waliokuwa mahututi, Hengaw ilisema.
Maandamano yanaendelea licha ya msako mkali ambao kundi la haki za binadamu la Iran lenye makao yake Oslo kusema Ijumaa kuwa waandamanaji 160 wameuawa, wakiwemo watoto zaidi ya darzeni mbili.
Takriban watu 93 waliuawa wkati wa maandamano tofauti ambayo yalizuka Septemba 30 katika mji wa kusini mashariki wa Zahedan juu ya riopoti za kubakwa kwa msichana tukio ambalo linadaiwa kufanywa na kamanda wa polisi, IHR imesema.
Kiasi cha wana usalama 20 wameuawa katika maandamano ya Amini, na wengine wanane huko Zahedan, kwa mujibu wa takwimu za AFP kulingana na ripoti rasmi.