Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema Jumatatu kwamba vikosi vya Russia nchini Ukraine vitashindwa kama vile vya Nazi vya Ujerumani vilivyoshindwa katika vita ya pili ya dunia.
"Tulipigana wakati huo na tunapigana hivi sasa, hakuna mtu yeyote kamwe atakayeyafanya mataifa mengine kuwa watumwa na kuharibu nchi nyingine", Zelenskyy alisema katika ujumbe wa video. Na maovu hayo yote ya zamani ambayo Russia ya sasa inayarudisha yatashindwa kama vile U-Nazi ulivyoshindwa.
Zelenskyy alisema lengo la Russia nchini Ukraine ni utumwa au uharibifu na alilinganisha uungwaji mkono ambao Ukraine imepokea kutoka mataifa mengine pamoja na juhudi za washirika ili kuishinda Ujerumani mnamo mwaka 1945.
Hotuba ya kiongozi huyo wa Ukraine pia ilijumuisha tangazo la amri ya kukumbukumbu ya ushindi wa Ujerumani hapo Mei 8 kama washirika wa magharibi wanavyofanya. Hiyo ni tofauti na Russia ambayo hufanya sherehe zake Mei 9.