Maamuzi ya mahakama kuu Marekani kuleta mvuto kwa wapiga kura Novemba-mchambuzi

Reagan Barklage wa St. Louis, na wanaharakati wengine wa haki za utoaji mimba wakiandamana mahakama kuu mjini Washington, Juni 27, 2016, wakati majaji walipoangusha sheria ya upingaji kutoa mimba ya Texas .

Mahakama kuu ya Marekani imepitisha haki za utoaji mimba na kuamua kwamba majimbo kote nchini hayana ruksa ya kuzuia haki za kikatiba kwa wanawake.

Majimbo mengi ya Kusini hasa katika jimbo la Texas waliweka sheria ya kufanya kuwa vigumu kwa wanAwake kutoa mimba.

Your browser doesn’t support HTML5

Mahojiano na Joel Ulomi.

Mchambuzi wa siasa nchini Marekani Bw.Joel Ulomi anaeleza huu ni uamuzi mkubwa sana hasa kwasababu sheria ya utoaji mimba imekuwa ikipingwa sana na majimbo yalioko kusini mwa Marekani.

Lakini kupingwa kwa sheria hiyo ya Texas na majimbo mengine ya kusini mwa nchi kutapelekea watoto wengi kuendelea kupoteza maisha watetezi wa sheria hiyo wameeleza.

Lakini mchambuzi anasema maamuzi haya yataleta mvuto wa aina yake kwa wafuasi wa vyama vya demokrat na republikan katika upigaji kura wa Novemba.