Watu hao wanasemekana kulazimishwa kupambana na watu wanaohusishwa na makundi ya kigaidi ya Al Qaida na Islamic State, mawakili, wanahabari pamoja na kundi la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch wamesema wiki hii.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, makundi hayo yanalaumu utawala wa kijeshi kwa kujaribu kunyamazisha uasi wa amani wakati ukijitahidi kurejesha hali ya usalama, kama ulivyoahidi wakati wa kuchukua madaraka kupitia mapinduzi ya Septemba 2022.
Mmoja wa wanachama wa shirika la wanahabari ambaye hakutaka kutambulishwa ameambia Reuters kwamba “ tumeanza kuona uso kamili wa utawala wa kijeshi, kwamba haujakuja kuokoa Burkina Faso.” Msemaji wa utawala huo hajajibu madai hayo hata baada ya kuombwa kufanya hivyo.