Utawala wa Biden unasema bado una matumaini kuhusu ombi la Sweden kujiunga na muungano wa usalama wa NATO licha ya maneno makali kutoka kwa mmoja wa wanachama muhimu wa NATO, Uturuki.
Lakini White House ilikataa kusema iwapo hilo linaweza kufanyika kabla ya mkutano wa NATO mwezi ujao. Ikiwa imesalia chini ya mwezi mmoja kabla ya NATO kukutana Julai 11 katika mji mkuu wa Lithuania, Vilnius, msemaji wa White House, Karine Jean-Pierre alisema Jumatano kwamba White House ina matumaini.
Bado tuna matumaini kwamba hili litafanyika, alieleza msemaji wa White House, Sina ratiba ya wakati, kwa hakika. Ni hivi karibuni, kama nilivyosema, bila kuchelewa. Kwa hivyo, tutaendelea kuwa wawazi. Tutaendelea kuwasiliana na Uturuki. Sweden inahitaji msaada wa pamoja kutoka kwa wanachama wote 31 wa NATO, kabla ya kujiunga.
Hadi sasa wanachama wote wamelikubali ombi la Sweden isipokuwa Hungary na Uturuki wamejitoa, na kupunguza matumaini kwamba Sweden inaweza kujiunga kabla, au wakati wa mkutano huo.