Viongozi wa upinzani nchini Ivory Coast wamesema kwamba wanaunda serikali ya mpito baada ya kususia uchaguzi mkuu uliofanyika jumamosi.
Wanasiasa hao walisusia uchaguzi huo baada ya rais Alassane Ouattara kugombea mhula wa tatu madarakani.
Hatua ya kutangaza kuunda serikali ya mpito inaongeza mgogoro zaidi baada ya nchi hiyo kuingia katika hali ya wasiwasi mwezi Agosti wakati Ouattara alipotangaza kwamba atagombea mhula mwingine madarakani.
Walitaja hatua ya Ouattara kuwa ukiukaji wa katiba na mapinduzi ya uchaguzi katika nchi hiyo ya Afrika magharibi.
Wanasiasa wakuu wa upinzani wamekataa matokeo ya uchaguzi yanayoonyesha kwamba rais Ouattara amepata ushindi mkubwa.
Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC