Upinzani nchini Guinea Bissau umeshinda kwa wingi uchaguzi wa wabunge

Raia wa Guinea Bissau wakishiriki katika zoezi la upigaji kura kwa wabunge

Muungano unaoongozwa na chama cha African Party for the Independence of Guinea and Cape Verde (PAIGC) ulishinda viti 54 kati ya 102 ukiongoza mbele ya chama cha Embalo Madem cha G15 ambacho kilipata viti 29 alisema Mpabi Cabi, kaimu mkuu wa tume ya uchaguzi

Upinzani nchini Guinea-Bissau umeshinda kwa wingi mkubwa wa viti katika uchaguzi wa bunge na hiyo ikiashiria kugawana madaraka na Rais Umaro Sissoco Embalo, kulingana na matokeo rasmi ya Alhamisi.

Muungano unaoongozwa na chama cha African Party for the Independence of Guinea and Cape Verde (PAIGC) ulishinda viti 54 kati ya 102, ukiongoza mbele ya chama cha Embalo Madem cha G15, ambacho kilipata viti 29 alisema Mpabi Cabi, kaimu mkuu wa tume ya uchaguzi.

Chama cha Social Renewal (PRS) kilishinda viti 12, Chama cha Workers kilipata viti sita, na kiti kimoja kilichukuliwa na Assembly of the People United. Taifa hilo dogo la Afrika Magharibi limekabiliwa na ukosefu wa utulivu kwa muda mrefu kutokana na mapinduzi ya mara kwa mara pamoja na matokeo ya uchaguzi yanayozozaniwa.